Isaiah 65:21-22


21 aWatajenga nyumba na kuishi ndani yake;
watapanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake.

22 bHawatajenga nyumba, nao watu wengine waishi ndani yake,
au kupanda mazao na wengine wale.
Kwa kuwa kama zilivyo siku za mti,
ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu,
wateule wangu watafurahia kwa siku nyingi
kazi za mikono yao.
Copyright information for SwhKC